Baba askofu Nestor Timanywa akishirikiana na Baba askofu Methodius Kilaini na mapadre zaidi ya 80 wamewaongoza mamia ya waamini kumuaga Marehemu Padre Deogratias Rugalama aliyezikwa leo katika makaburi ya mapadre yaliyo katika Seminari ya Rubya. Padre Deogratias alikuwa mpenda watu, mpenda maendeleo na aliyejitoa bila kujibakiza katika kuwahudumia watu bila hata kujali afya yake mwenyewe. Sisi tulimpenda lakini Mungu amempenda zaidi. Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio katika Ibada ya kumsidikiza Marehemu Padre Deogratias Rugalama.
Padre Deogratias Rugalama
Alizaliwa 06/09/1956
Upadrisho 13/01/1985
Kufa 19/11/2011
1 comment:
Waitu Mutai n'akashengo. Omukama asinge amuumuze n'emilembe.
Fr. Felix Mushobozi, CPPS
Post a Comment