KARIBU KWENYE BLOGU YA BAWA

Toa maoni, ushauri, habari, mapendekezo n.k. katika kuboresha BAWA.

Bonyeza sehemu iliyoandikwa comment/maoni kila baada ya post na kisha andika ujumbe wako.

Asante kwa ushirikiano wako.

Sunday, December 25, 2011

Heri ya Krismas


Tunawatakia wanaBAWA na wote wanaofuatilia hii blog yetu heri na baraka za sherehe hii ya kuzaliwa Bwana.

Sunday, December 11, 2011

Hongera sana Pd. Remigius Rutashubanyuma

Wanaparokia ya Buyango, Jimbo Katoliki la Bukoba, wanayo furaha kubwa kumpokea padre mpya Pd. Remigius Rutashubanyuma mzaliwa wa parokia hiyo aliyepewa daraja la Upadre leo katika Kanisa la Parokia hiyo. Zifuatazo ni picha za kumbukumbu katika tukio hilo muhimu.











Sunday, December 4, 2011

Hongera sana Pd. Samuel Muchunguzi

Ilikuwa furaha na nderemo katika parokia ya Kishogo, Jimbo katoliki la Bukoba alipopadrishwa aliyekuwa Shemasi Samuel Muchunguzi siku ya leo. Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio katika sherehe hizo za Upadrisho wa Pd. Samuel Muchunguzi.













Saturday, December 3, 2011

Hongera Sana Pd. Prophilio Mulokozi

Leo Parokia ya Bukoba, Jimbo Katoliki la Bukoba, imebarikiwa kumpata Padre mpya mzaliwa wa Parokia hiyo. Mh. Padre Prophilio Mulokozi Hongera sana. Zifuatazo ni picha kadhaa katika tukio hilo la Upadrisho huo.










Saturday, November 26, 2011

MHASHAMU BABA ASKOFU GERVASE NYAISONGA( JIMBO LA DODOMA) ATOA HUDUMA ZA USOMAJI NA UTUMISHI ALTARENI KATIKA SEMINARI KUU YA MT PAULO - KIPALAPALA








Mafrateri 18 wa Mwaka II wapewa Huduma ya Usomaji(Lectorship) na 19 wa Mwaka III Utumishi Altareni(Acolyte).
Kwa Upande wa BAWA-Mafrateri, Almachius Rwejuna amepata huduma ya Usomaji, Philbert Mutalemwa na Viator Mujuni wamekuwa Watumishi Altareni. Tunamshukuru Mungu kwa hatua hii walioifikia Mafrateri wetu na tunawaombea Wito Kamilifu.

Tuesday, November 22, 2011

Marehemu Padre Deogratias Rugalama, apumzike kwa amani.

Baba askofu Nestor Timanywa akishirikiana na Baba askofu Methodius Kilaini na mapadre zaidi ya 80 wamewaongoza mamia ya waamini kumuaga Marehemu Padre Deogratias Rugalama aliyezikwa leo katika makaburi ya mapadre yaliyo katika Seminari ya Rubya. Padre Deogratias alikuwa mpenda watu, mpenda maendeleo na aliyejitoa bila kujibakiza katika kuwahudumia watu bila hata kujali afya yake mwenyewe. Sisi tulimpenda lakini Mungu amempenda zaidi. Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.


Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio katika Ibada ya kumsidikiza Marehemu Padre Deogratias Rugalama.










Padre Deogratias Rugalama 
Alizaliwa 06/09/1956
Upadrisho 13/01/1985
Kufa 19/11/2011