KARIBU KWENYE BLOGU YA BAWA

Toa maoni, ushauri, habari, mapendekezo n.k. katika kuboresha BAWA.

Bonyeza sehemu iliyoandikwa comment/maoni kila baada ya post na kisha andika ujumbe wako.

Asante kwa ushirikiano wako.

Saturday, November 26, 2011

MHASHAMU BABA ASKOFU GERVASE NYAISONGA( JIMBO LA DODOMA) ATOA HUDUMA ZA USOMAJI NA UTUMISHI ALTARENI KATIKA SEMINARI KUU YA MT PAULO - KIPALAPALA








Mafrateri 18 wa Mwaka II wapewa Huduma ya Usomaji(Lectorship) na 19 wa Mwaka III Utumishi Altareni(Acolyte).
Kwa Upande wa BAWA-Mafrateri, Almachius Rwejuna amepata huduma ya Usomaji, Philbert Mutalemwa na Viator Mujuni wamekuwa Watumishi Altareni. Tunamshukuru Mungu kwa hatua hii walioifikia Mafrateri wetu na tunawaombea Wito Kamilifu.

Tuesday, November 22, 2011

Marehemu Padre Deogratias Rugalama, apumzike kwa amani.

Baba askofu Nestor Timanywa akishirikiana na Baba askofu Methodius Kilaini na mapadre zaidi ya 80 wamewaongoza mamia ya waamini kumuaga Marehemu Padre Deogratias Rugalama aliyezikwa leo katika makaburi ya mapadre yaliyo katika Seminari ya Rubya. Padre Deogratias alikuwa mpenda watu, mpenda maendeleo na aliyejitoa bila kujibakiza katika kuwahudumia watu bila hata kujali afya yake mwenyewe. Sisi tulimpenda lakini Mungu amempenda zaidi. Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.


Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio katika Ibada ya kumsidikiza Marehemu Padre Deogratias Rugalama.










Padre Deogratias Rugalama 
Alizaliwa 06/09/1956
Upadrisho 13/01/1985
Kufa 19/11/2011



Sunday, October 30, 2011

HIJA NYAKIJOOGA 2011

Kulingana na utaratibu wa kila mwaka, hufanyika Hija kwa Mama Bikira Maria huko Nyakijooga - Lurdi ya Bukoba katika Jumapili ya mwisho ya mwezi wa Rozari yaani mwezi wa kumi. Mwaka huu imefanyika tarehe 30/10/2011. Mahujaji walikuwa wengi waliokuja kujipatia neema za Hija hii. Waliweza kupata mafundisho safi kabisa juu ya Bikira Maria yaliyotolewa na Mha. Methodius Kilaini, Askofu Msaidizi wa Bukoba pamoja na kushiriki ibada yenye utulivu wa aina yake iliyoongozwa na Mha. Nestor Timanywa, Askofu wa Jimbo la Bukoba akishirikiana pia na Mha. Almachius Rweyongeza, Askofu wa Jimbo la Kayanga, pamoja na mapadre wengi wa Jimbo la Bukoba. Mahujaji walitolea sala na shukrani (ekishisha) kwa Mama Bikira Maria ambavyo vilionyesha imani kubwa waliyo nayo kwa maombezi ya huyu Mama wa Mungu na Mama yetu. Yafuatayo ni baadhi matukio katika picha ya Hija ya mwaka huu.






















BIKIRA MARIA, MALKIA WA ROZARI TAKATIFU
UTUOMBEE

Friday, October 28, 2011

PADRE ALIYEVUNJA REKODI YA KUISHI MIAKA MINGI - BUKOBA, AAGA DUNIA.


Si mwingine bali ni Padre Desiderius Kashangaki mzaliwa wa Parokia ya Kanyigo. Aliyezaliwa tarehe 23/05/1911 na kuaga dunia tarehe 26/10/2011 akiwa na umri wa miaka 100 na miezi mitano. Haya ni baadhi ya matukio katika ibada ya mazishi yake iliyofanyika tarehe 28/10/2011 huko Rubya.











APUMZIKE KWA AMANI. AMINA!

Thursday, October 20, 2011

NYAKUTUNUNTA POLYCARP PENGO YATUNGA ABAFURATERA EMYOGA Y'OBUSHOMI(LECTORSHIP) N'OBUHEREZA ALTARI(ACOLYTE) OMU SEMINARI NKURU - SEGEREA

Ta Nyakutununta Polycarp Pengo hamoi n'Abafuratera bashatu ba BAWA abatungire emyoga y'Obushomi n'Obuhereza omu Seminari Nkuru y'Omutakatifu Carol Lwanga- Segerea. Omu bulyo bwa Ta Nyakutununta ni Frt Dionysius Rwamugira(Mwaka III) atungirwe omwoga gwo Obuhereza;
omu bumosho bwe bafuratera Principius Kamuhabwa(Mwaka II) aina omukanda gulikwiragura, atungirwe omwoga gw'Obushomi, alikuhonderaho ni Emmanuel Kamugisha(Mwaka III) atungirwe omwoga gw'Eihereza.
Abana BAWA nitubagondeza emilembe kakeka omurugendo rwanyu, Omukama wenene abememu mugume mugizire orwoyoyo rw'okumukorera kurungi nk'Abasaserdoti be. Omukama alinde! Kandi mara Ma Bikira Maria Omukama w'Entumwa atushabire!

Thursday, October 6, 2011

MHE. PD. ADEODATUS RWEHUMBIZA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MAFRATERI - BAWA KIPALAPALA SEMINARI KUU(2011/2012)

Ni baada ya kuongoza mafungo ya mwaka kwa mafrateri wa Seminari Kuu Kipalapala - Tabora
Kulia kwa Fr. Adeodatus(aliyeko katikati) ni Mafrateri: Philbert Mutalemwa(Mwaka III), Ericus Shumbusho( Mwaka I) na Deodatus Katunzi(Mwaka IV)
Kushoto kwake ni Mafrateri: Viator Mujuni( Mwaka III), Evodius Mwijage (Mwaka IV) na Almachius Rwejuna( Mwaka II)