Kulingana na utaratibu wa kila mwaka, hufanyika Hija kwa Mama Bikira Maria huko Nyakijooga - Lurdi ya Bukoba katika Jumapili ya mwisho ya mwezi wa Rozari yaani mwezi wa kumi. Mwaka huu imefanyika tarehe 30/10/2011. Mahujaji walikuwa wengi waliokuja kujipatia neema za Hija hii. Waliweza kupata mafundisho safi kabisa juu ya Bikira Maria yaliyotolewa na Mha. Methodius Kilaini, Askofu Msaidizi wa Bukoba pamoja na kushiriki ibada yenye utulivu wa aina yake iliyoongozwa na Mha. Nestor Timanywa, Askofu wa Jimbo la Bukoba akishirikiana pia na Mha. Almachius Rweyongeza, Askofu wa Jimbo la Kayanga, pamoja na mapadre wengi wa Jimbo la Bukoba. Mahujaji walitolea sala na shukrani (ekishisha) kwa Mama Bikira Maria ambavyo vilionyesha imani kubwa waliyo nayo kwa maombezi ya huyu Mama wa Mungu na Mama yetu. Yafuatayo ni baadhi matukio katika picha ya Hija ya mwaka huu.
BIKIRA MARIA, MALKIA WA ROZARI TAKATIFU
UTUOMBEE
2 comments:
Nawashukuru wana BAWA kwa kuleta taarifa nzuri hii ya hija. Nilikuwa mmojawapo wa walioshiriki hia hiyo. Naomba uendelee kueneza ujumbe huu kwa wengi zaidi. Kumbe BAWA inaendelea! Nilishiriki kuiandika miaka ya 70. Hongera wana BAWA.
p.kashangaki-Loyola Dar.
Asante sana kwa kututia moyo. Mwenyezi Mungu akubariki sana.
Post a Comment