KARIBU KWENYE BLOGU YA BAWA

Toa maoni, ushauri, habari, mapendekezo n.k. katika kuboresha BAWA.

Bonyeza sehemu iliyoandikwa comment/maoni kila baada ya post na kisha andika ujumbe wako.

Asante kwa ushirikiano wako.

Saturday, December 25, 2010

Heri ya Krismas!

Nachukua fursa hii kuwatakieni nyote heri na baraka za sherehe ya kuzaliwa Bwana wetu Yesu Kristo.


MERRY CHRISTMAS.

Waitu Mwaihyuka na NOEL

Ninkwasa obushango obu kubaihyukya inywena n'ekiro kikuru ky'Okuzarwa Omukama waitu Yezu Kristu.
Waitu mwaihyuka na NOEL.

Friday, December 24, 2010

Planned Event by Bishop Nestor Timanywa

Baba Askofu Nestor Timanywa anawaalika wana-Bukoba wanaoishi nje ya jimbo washeherekee naye Christmas tarehe 27 Desemba 2010, Jumatatu.

RATIBA:


Ibada ya Misa saa 4 Asubuhi
Mlo wa sikukuu
Burudani ya Bukoba (KAKAU) hadi jioni

Nia ni kusali pamoja, kuongea, kujuana ili kushirikiana na kusheherekea.

Kuchangia gharama ni Tsh. 25,000/- tu kwa kichwa.
Itafanyika Balamaga – Kolping Hotel. Usafiri utakuwepo kutoka na kurudi mjini na bandarini kwa meli.

NB. Patakuwepo na children’s corner kwa watoto. Anayetaka malazi yanapatikana hapo Kolping Hotel, book. Vinywaji baridi vitapewa, (na vinywaji moto bar itakuwepo).

Nafasi ni 250 tu fanya booking yako mapema kwa:

Askofu Method Kilaini
Tel. +255713262836; +255756146449
e-mail: mkilaini@gmail.com

Fr. Adeodatus Rwehumbiza
Tel. +255783176303
e-mail: b.officebk@yahoo.com

au: Mr. Venant Mpanju
Coordinator Kolping Tanzania
Tel. +255713220953
kst@kolpingtanzania.com

Monday, December 13, 2010

Hongera Padre Patience Mutalemwa

WanaBAWA tunazidi kumshukuru Mungu aliyetuzawadia Padre mpya mwanaBAWA kwa mara nyingine tena, naye ni Padre Patience Mutalemwa aliyepadrishwa leo huko Parokiani Mwemage, Jimboni Bukoba.
Fr. Patience Mutalemwa, waitu waihyuka muno!

Sunday, December 12, 2010

TANZIA

WanaBAWA tunaungana na mwanaBAWA mwenzetu Frt. Evodius Mwijage aliyempoteza mama yake mpendwa Ma. Godeliva Kokuhirwa aliyeaga dunia leo. Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani.
BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LITUKUZWE!

Hongera Padre Switbert Mujuni





WanaBAWA tunaendelea kumshukuru Mungu kwa zawadi ya miito katika Kanisa lake tunapoungana tena kumpongeza mwanaBAWA aliyepewa daraja la Upadre leo huko parokiani Rukindo.
Fr. Switbert, waitu waihyuka muno!

Sunday, December 5, 2010

Hongera Padre Erick Muganyizi na Padre John Philip Karumuna



















WanaBAWA tunaendelea kumshukuru Mungu kwa kutujalia mapadre wapya wengine wawili waliopadrishwa leo huko parokiani Kagondo na Mha. Nestori Timanywa, Askofu wa Jimbo la Bukoba.
Fr. Erick na Fr. John Philip waitu baihyuka muno!

Hongera Padre Dionysius Muchunguzi

WanaBAWA tunaungana kumpongeza padre mpya mwanaBAWA aliyepadrishwa leo huko parokiani Rubya, Bukoba na Mha. Nestori Timanywa, Askofu wa Jimbo katoliki la Bukoba.
Waitu Baihyuka Muno.
Congratulations Rev. Fr. Dionysius Muchunguzi