Pages
KARIBU KWENYE BLOGU YA BAWA
Toa maoni, ushauri, habari, mapendekezo n.k. katika kuboresha BAWA.
Bonyeza sehemu iliyoandikwa comment/maoni kila baada ya post na kisha andika ujumbe wako.
Asante kwa ushirikiano wako.
Bonyeza sehemu iliyoandikwa comment/maoni kila baada ya post na kisha andika ujumbe wako.
Asante kwa ushirikiano wako.
BUKOBA DIOCESE WEBSITE
Saturday, September 24, 2011
Tuesday, September 6, 2011
Msgr. Sylvester Rutabanzibwa hatunaye tena!!
Jimbo la Bukoba na Kanisa kwa ujumla limepoteza hazina kubwa! Ni hayati Msgr. Sylvester Rutabanzibwa aliyefariki dunia tarehe 03/09/2011 hospitalini Kagondo na kuzikwa leo katika makaburi ya mapadre - Rubya seminari.
Msgr. Sylvester alikuwa padre mwema, aliyejitoa bila kujibakiza, alisimamia ujenzi wa makanisa ya Kijwire, Katoma, Rutabo pamoja na nyumba za mapadre huko Katoma na Rutabo. Alihudumia kwa kiaminifu katika nafasi mbalimbali na muhimu katika jimbo la Bukoba, pia alifanya mambo mengine mazuri ambayo hatuwezi kuyataja yote hapa. Kwa ufupi kwa msemo wa wakati huu, Msgr. Sylvester alikuwa ni JEMBE la Jimbo.
Bwana alitoa, na Bwana ametwaa, Jina la Bwana litukuzwe.
APUMZIKE KWA AMANI!
Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio katika ibada ya kumsindikiza hayati Msgr. Sylvester Rutabanzibwa
Jeneza lililoubeba mwili wa hayati Msgr. Sylvester likiwa katika kanisa la Parokia ya Rubya tayari kwa Ibada ya Mazishi. |
Baba Askofu Nestor Timanywa na Baba Askofu Almachius Rweyongeza wakitoa heshima zao kwa mwili wa Hayati Msgr. Sylvester. |
Mwili wa hayati Msgr. Sylvester ndani ya jeneza kabla ya kupelekwa makaburini. |
Baba Askofu Nestor Timanywa akiweka udongo katika Kaburi la hayati Msgr. Sylvester |
Jeneza lililoubeba mwili wa Hayati Msgr. Sylvester katika kaburi lake |
|
|
|
Baba Askofu Nestor Timanywa akimalizia Ibada ya mazishi ya hayati Msgr. Sylvester |
Kaburi la Msgr. Sylvester Rutabanzibwa.
Kuzaliwa 27/10/1922
Upadrisho : 13/07/1952
Umonsinyori: 23/02/1999
Kufariki: 03/09/2011
Kuzikwa: 06/09/2011
RIP
Subscribe to:
Posts (Atom)